Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua mchunga ng’ombe

Anyongwa Picg Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua mchunga ng’ombe

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyoketi Wilayani Mufindi imemhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa, Mkazi wa Kijiji cha Mtambula Wilayani Mufindi Liston Lugange (33) baada ya kukutwa na hatia ya kosa la mauaji ya kukusudia dhidi ya Emmanuel Mbigi (19) alikuwa mfanyakazi wa kuchunga ng’ombe kwa Donald Chelesi.

Katika shauri hilo washtakiwa walikuwa wawili ambapo mshtakiwa wa kwanza amehukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa huku mshtakiwa wa pili Oscar Tefu (29) akiachiwa huru baada ya mahakama hiyo kujilidhisha na ushaidi ambao ulitolewa mbele yake Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Iringa iliyoketi Wilaya Mufindi, Ilvin Mgeta.

Awali ilielezwa kuwa mahakamani hapo mshtakiwa, Listoni Lugange alikamatwa June 5, 2019 katika Kijiji cha Igowole wakati alipokuwa katika harakati za kuuza ngo’ombe ndipo mtego uliwekwa baina ya aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mtambula Octavian Kalinga.

Ofisa Mtendaji huyo baada ya kushtukia kuwa ng’ombe hao huenda wangekuwa wa wizi kutokana na Liston Lugange kugomea kwenda kuandikishana ili kuweza kufanya mauzo ya kuuziana ng'ombe hao.

Baada ya mtego huo mshtakiwa huyo alifika kijijini hapo kwa ajili ya kufanya biashara ya ng’ombe hao ndipo alipokamatwa na kufikishwa mahakamani hapo na alipoulizwa kuhusu shikta hilo alikana  kutenda kosa hilo ndipo upande wa mashtaka ukalazimika kuleta mashahidi watano  na vielelezo viwili kwa ajili ya kuthibitisha.

Pia imeelezwa mahakamani hapo Lugange alitenda kosa hilo mnamo June 4,2019 majira ya saa 6 za mchana  huko kijijini kwao Mtambula baada ya ya kuiba ng’ombe wawili  aina ya maskai na kumuuliza marehemu kama anamfahamu ambapo marehemu alikiri kumtambua na ndipo alipompiga na kitu kizito kichwani kisha kumkata sikio lake la kulia na kumtelekeza porini baada ya kugundua kuwa amefariki.

Hivyo, akizungumza kabla ya hukumu hiyo, mwendesha mashtaka wa Serikali Yahaya Misango amesema kwa upande wa mashtaka hawana kumbukumbu zozote zinazoonyesha mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.

Misango amesema kuwa mahakama imemtia hatiani mshtakiwa wa kwanza chini ya kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura 16 ambayo ilifanyiwa marejeo mwaka 2022 ambapo sheria kwa kosa la mauaji ya kukusudia.

"Kwa msingi huo upande wa mashta unaiomba mahakama yako ijielekeze katika kifungu namba 197 cha kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022 katika kutoa adhabu kwa mshtakiwa ambaye amekutwa na hatia kama hiyo." amesema Misango

Kwa  upande wa utetezi wa mshtakiwa ukiongozwa na Wakili Cosmas Kishamawe umeieleza mahakama kuwa mteja wake amekutwa na hatia ya kutenda kosa hilo na ukizingatia kosa hilo halina adhabu mbadala hivyo kwa upande wake hawana maombolezo juu ya shauri hilo.

Shauri hilo la mauaji namba 10/2019 ambalo hukumu yake ilitolewa jana Jumatatu March 27, 2023 na Jaji Mgeta wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyoketi Wilaya hapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: