Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Lebron, Curry wamsuta Ant Man

Steph X Lebron Lebron, Curry wamsuta Ant Man

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Jamaa amekubali. Kabla ya kuanza kwa michuano ya Olimpiki nchini Ufaransa, nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Anthony Edwards 'Ant Man' alitoa kali, kwamba wachezaji wenzake wa timu ya Taifa hilo, watalazimika kucheza kumzunguka yeye.

Ant Man alitoa kauli hiyo ambayo licha ya kushangaza wengi lakini walichukulia poa kutokana na alivyokua na tambo kwenye mechi za mchujo (playoffs) Ukanda wa Magharibi msimu uliopita.

Hata hivyo, mchezo wa mwisho wa kundi dhidi ya Puerto Rico, Ant Man aliyefunga pointi 26 aliishia kuchutama kwa kukiri wazi, hakuna wachezaji bora kwake kama mastaa hao, LeBron, Curry na KD kutokana na ubora wao na ulikuwa sababu ya yeye kung'ara kwenye mchezo huo.

Ant Man alikuwa gumzo kwenye mechi za mtoano hasa alivyoupiga mwingi dhidi ya aliyekua bingwa mtetezi Denver Nuggets ya Nikola Jokic na kuwavua taji, alikuwa anajigamba vilivyo na alifanikiwa kuzua gumzo.

Safari hii aliamua kuwaweka pembeni mastaa wakubwa wa NBA, Steph Curry, Kevin Durant na LeBron James watatakiwa kuwa chini yake kiuchezaji ili Marekani itwae taji la Olimpiki inayoendelea pale Paris Ufaransa kabla ya kuukubali mziki wao.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: