Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nikifanya Amapiano nitawapoteza mno - Alikiba

Kiba Wazi Nikifanya Amapiano nitawapoteza mno - Alikiba

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfalme wa Bongo Flava, Alikiba hatimaye amejibu kuhusu ni kwa nini amekaa kimya bila kufanya wimbo kwa mtindo wa Amapiano ambao unafagiliwa kwa kasi kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Alikiba alifunguka haya akimjibu shabiki wake mmoja kwenye Twitter ambaye aliuliza kama kweli msanii huyo amewahi fanya wmbo wowote kwa mdundo wa Amapiano.

Alikiba alitema cheche kali za vitisho akisema kuwa tayari ameshapewa changamoto na wasanii chipukizi ambao wanafanya vizuri Bongo Flava kwa midundo ya Amapiano.

Kwa mujibu wa King Kiba, wasanii hao wamempa challenge lakini alisema kuwa iwapo ataikubali kuzichapa nao kwenye mduara wa midundo ya Amapiano, basi atawatokomeza kabisa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

“Hivi Alikiba ana ngoma hata moja ya Amapiano kweli?” aliuliza mdau mmoja kwa jina Irene Igora.

Akimjibu, Alikiba aliandika;

“Marioo na Chino Wana Man wameni challenge nifanye. Onyo kwa wadogo zangu. Nitawapoteza huko huko kwenye uwanja wao wa nyumbani,” Alikiba alijibu.

Alikiba anatangaza mkwara huu ikiwa ni siku chache baada ya mshindani wake wa muda mrefu Diamond Platnumz pia kutema mikwara mingi kuhusu ujio wake kwenye ngoma ikiwa ni miezi kadhaa tangu alipoachia kibao cha mwisho.

Msanii huyo kwa kuonesha kwamba anamaanisha maneno yake, aliachia mdundo Fulani unaokaa Amapiano hivi na kusema kwamba ni kionjo cha ngoma yake ‘Shuu’ ambayo inatarajiwa kushuka muda wowote hivi karibuni.

Wengi wamekumbatia challenge hiyo yenye sauti ya mdundo tu wala hajatoa sauti ya wimbo wenyewe.

Kwa upande wake, Marioo amekuwa akifanya vizuri pakubwa kwa midundo ya Amapiano ambapo wengi wamemtaja kuwa ndiye msanii pekee wa Tanzania aliyefanikiwa pakubwa kwa kuimba nyimbo kadhaa za mdundo huo wenye asili ya Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: