Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rich One amchana Alikiba ishu ya madai ya Timbulo kutapeli

Rich One Kiba Timbulo Dsc Rich One amchana Alikiba ishu ya madai ya Timbulo kutapeli

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara na Meneja wa wasanii mbalimbali Bongo, Rich One amekanusha taarifa iliyotolewa na supastaa wa Bongo Fleva kuhusu tuhuma utapeli anaodaiwa kuufanya msanii Timbulo kwa kutumia jina la Kiba.

Alikiba siku ya Miaka 20 ya Mfalme wikiendi iliyopita alisema kwamba Timbulo aliwahi kuchukua pesa ya shoo ya Alikiba miaka ya nyumba, akawadanganya mashabiki kuwa yeye ni Kiba, kwa mujibu wa Rich One amefunguka kuwa sio kitu cha kweli.

"Kaeni mkielewa kuwa kati ya Timbulo na Alikiba ni Timbulo ndiye aliyeanza kutoka kumuziki, sasa iweje leo Alikiba aje kusimama aseme Timbulo kajifanya Alikiba kwenye shoo.

"Timbulo alianza kubadili nyimbo za nje kuzifanya kwa Kiswahili na zikfanya vizuri akawa mkubwa, Alikiba kaongea upuuzi," amesema Rich One.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: