Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi yamsaka mchungaji aliyeagiza waumini wafunge, wafe

Polisi Ew Polisi yamsaka mchungaji aliyeagiza waumini wafunge, wafe

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi katika Kaunti ya Malindi nchini Kenya linamtafuta Mchungaji Paul Mackenzie wa Kanisa la Good News International kutokana na kudaiwa kuwashawishi waumini wake wafunge kisha wafe ili waweze kuingia mbinguni na kuurithi ufalme.

Taarifa za awali zinaeleza waumini wanne wamefariki wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali Kuu Kaunti Ndogo ya Malindi, huku mmoja amefariki baada ya kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Lango Baya ambako walipelekwa kwa ajili ya kutoa maelezo.

Polisi wamefanya msako baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu kuwepo kwa kanisa hilo lenye kueneza imani potofu kwa kuelekeza watu kufunga kisha wafe ili waweze kufika mbinguni.

Wakazi wa eneo la Shakahola, Kata ya Adu wamesema kwamba mhubiri huyo amekuwa akiwashawishi waumini wake wafunge bila kula, wafe ili waweze kuurithi ufalme wa mbinguni.

Tovuti ya Taifa Leo nchini Kenya ilieeleza kuwa, matukio ya imani potofu yameongezeka, huku polisi wakiahidi kumkamata Mchungaji huyo kutokana na kusambaza imani hiyo potofu.

Miongoni mwa maelezo yaliyoandikishwa polisi na wananchi waliotoa taarifa inadaiwa kuna kaburi la pamoja lenye miili 31 ya waathirika wa mafundisho hayo potofu eneo la Shakahola.

Maafisa wa usalama waliofika eneo la Shakahola jana Alhamisi Aprili 13, 2023 waliwaokoa watu 15 ambao kati ya hao 6 wamepelekwa hospitalini kutokana na kudhoofika kiafya na wanne inaelezwa walipoteza maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: