Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjane wa Gaddafi akata rufaa mabilioni ya mumewe yasirudishwe Libya

Batch Safia Farkash M Mjane wa Gaddafi, Safiya Ferkash

Sun, 24 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjane wa aliyekuwa Rais wa Libya Hayati Muammar Gaddafi amekata rufaa ya maamuzi ya Mahakama ya nchini Malta iliyoidhinisha kiasi cha Euro milioni 95 zilizokuwa zimehifadhiwa katika Benki Kuu ya Nchi hiyo kurudishwa katika Serikali ya nchi ya Libya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama Kuu ya nchi hiyo ni kwamba kiasi hicho cha fedha kilihifadhiwa na aliyekuwa mtoto wa Gaddafi, Mutassim Gaddafi ambaye naye aliuawa wakati wa vita ya kumuondoa madarakani Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Safiya Ferkash pamoja na mwanasheria wake wamesema Mahakama ya Malta haina ushahidi wa kutosha na hivyo hawana uwezo wa kuruhusu pesa hiyo irudi nchini Libya.

Hukumu ilitolewa mwezi Juni mwaka huu ikiwa ni baada ya kipindi cha miaka 10 cha mapambano ya kisheria.

Rufaa hiyo imekatwa kwa niaba ya mrithi wa Gaddafi na Mwanasheria kutoka nchini Malta, Louis Cassar Pullicino ingawa hadi sasa haijawekwa wazi ni lini rufaa hiyo itasikilizwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: