Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuriko yasomba kambi ya wahanga wa tetemeko

Cs Mafuriko Asgsags Mafuriko yasomba kambi ya wahanga wa tetemeko

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafuriko yameharibu kambi za wahanga wa tetemeko la ardhi nchini lililoikumba Syria hivi karibuni.

Wahanga hao walihamishiwa katika kambi hiyo baada ya nyumba zao kuharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea Februari 6 mwaka huu na kuua maelfu ya watu.

Zaidi ya matenti 300 yaliyopo katika kambi 20 zinazohifadhi waathirika hao wa tetemeko la ardhi zimebomolewa na mvua hiyo.

Wizara ya ulinzi ya Syria imesema mvua hiyo kubwa imesababisha barabara nyingi kushindwa kupitika.

Wizara hiyo imesema suluhisho kwa waathirika hao ni kurejea katika nyumba zao badala ya kuendelea kuishi katika makambi hayo.

Mmoja wa waathirika Askarah Al- Muhammad amesema ” nilikuwa na wanangu ndani ya tenti wakati mvua inaanza kunyesha na vitu vyetu vyote vimechukuliwa na maji,”.

” Nilipoteana na wanangu kwa masaa kadhaa kwa sababu ya taharuki,” ameongeza.

Zaidi ya familia 223 zimeripotiwa kukosa nyumba za kuishi katika makambi hayo baada ya tenti zao za dharura kusombwa na maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: