Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ilivyo Nairobi, polisi watinga mtaani na farasi

Farasi Kenya Sd.jpeg Hali ilivyo Nairobi, polisi watinga mtaani na farasi

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shughuli mbalimbali zimesimama katika jiji la Nairobi nchini Kenya, huku askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakitumia mabomu ya machozi kusambaratisha maandamano ya upinzani.

Mapambano makubwa baina ya askari na waandamanaji hao yameonekana katika mtaa wa Kenyatta ambapo baadhi ya waandamanaji wamekuwa wakiwarushia mawe askari walioonekana kupambana nao.



Maandamano nchini Kenya yameitishwa na Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga kwa madai ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha na utawala wa Rais William Ruto wa Taifa hilo.

Akitangaza kufanyika kwa maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika leo, Odinga alisema itakuwa ni siku ya mapumziko ili wananchi wengi waweze kushiriki.



Hata hivyo Rais Ruto alisema hakutakuwa na maandamano hayo na kwamba siku ya leo ni siku ya kazi kama kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: