Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gari la Maiti latumika kusafirisha Bangi, harufu yawakamatisha

Gari La Maiti Bangi Gari la Maiti latumika kusafirisha Bangi, harufu yawakamatisha

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Kenya, wamefanikiwa kukamata shehena ya magunia 12 ya bangi, yaliyokuwa yakisafirishwa kupelekwa Kisumu kwa gari la kubebea maiti.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kaunti ya Busia, Maxwell Nyaema amesema gari hilo la Rafiki Funeral Services-Othaya, lilikamatwa baada ya kusimamishwa kwa ukaguzi wa kawaida.

Amesema, ” sasa dereva aliposhusha dirisha, Afisa wa Polisi aligundua harufu isiyokuwa ya kawaida na baada ya upekuzi waliyaona magunia hayo yamepangwa sehemu ya kuweka jeneza.

Kufuatia tukio hilo, Kamanda Nyaema amesema Polisi haitasita kuwachukulia hatua watu wote wanaoenda kinyume na taratibu au sheria zilizowekwa, huku akiwasihi wahalifu kutafuta njia salama za kujitafutia kipato.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: