Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajiua kukwepa rushwa ya sh 520,000 polisi

Maiti Ajiua kukwepa rushwa ya sh 260,000 polisi

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume wa miaka 40, mkazi wa Kijiji cha Manyata katika Kaunti ya Murang’a nchini Kenya, anadaiwa kujiua akikwepa deni la KSh30, 000 (sawa na Sh520, 000 za Tanzania) ambalo linadaiwa kuwa rushwa kwa polisi wa Kituo cha Sabasaba.

Kwa mujibu wa msemaji wa kamati ya marafiki kuhusu maziko ndugu huyo aliyejulikana na kwa jina la Joseph Murigi, imeelezwa kuwa polisi hao walikuwa wakimdai hongo hiyo, ili wasimshtaki kwa hatia ya kupakia picha za ‘aibu’ mitandaoni.

“Murigi alikuwa na kashfa fulani kutoka kwa mpenzi wake. Picha za chafu za mpenzi huyo zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii na akatajwa kama mshukiwa mkuu,” amesema James Guchu ambaye ni msemaji wa kamati hiyo.

Guchu aliongeza kuwa, baada ya mwanamke huyo kuripoti katika kituo cha polisi cha Sabasaba, Murigi alianza kutafutwa ili atiwe mbaroni.

“Polisi walifanikiwa kumkamata na kumfikisha kituoni kwao hapo Sabasaba, ambapo kesi iliandaliwa kienyeji na hivyo kukutwa na hatia. Aliamriwa kulipa faini ya Sh30, 000; ambazo zilikuwa zikabidhiwe kwa mkuu wa kituo,” amesema.

Kwa kuwa marehemu hakuwa na fedha hizo, inadaiwa kwamba baadhi ya marafiki na familia kwa pamoja walichangishana papo kwa papo na kufanikiwa kupata Sh15, 000.

“Murigi aliachiwa kwa dhamana hata hivyo alitakiwa kumalizika pesa iliyokuwa imebaki kabla ya Agosti 7, 2023. Hata hivyo, marehemu alisistiza kuwa, hakusuika katika kusambaza picha hizo na kwamba ametiwa hatiani bila kuwa ushahidi wa kumhusisha kutolewa,” amesema Guchu.

Kwa upande wake, Evanson Njogu ambaye ni baba wa marehemu, ameiambia Taifa Leo Dijitali, kwamba alipigiwa simu na maofisa wa polisi wa Nanyuki Agosti 10, mwaka huu; akielezwa kuwa mwanae alikuwa amejinyonga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: