Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga watoa taarifa alipo Mkude (+Video)

Video Archive
Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam mapema leo Jumapili kikitokea Mwanza, huku kocha mkuu wake Miguel Gamondi akizungumzia mikakati yake kuelekea mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imerejea ikiwa imevuna alama tatu na mabao manne katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold pale CCM Kirumba, Mwanza. Pia ilikutana na kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Ihefu. Msimu uliopita Yanga ilichezea kichapo mbele ya Ihefu na kuvunjwa kwa rekodi yake ya kutopoteza mchezo kwenye ligi.

Kipigo dhidi ya Ihefu ni cha kwanza kwa Yanga kwenye Ligi Kuu msimu huu.

Mbali na Gamondi kuzungumzia mikakati yake kwenye michuano hiyo, Mratibu wa klabu hiyo Hafidhi Saleh amefafanua ni wapi walipo kiungo Jonas Mkude na Metacha Mnata ambao, katika siku za karibuni wamekuwa hawaonekani kikosini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: