Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Prince Dube: Wananchi mtafurahi

Prince Dube Yanga Hsz Prince Dube

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa Prince Dube limetosha kuipa ushindi wa 0-1 klabu ya Yanga yenye maskani yake eneo la Jangwani nchini Tanzania, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya TX Galaxy ya Afrika Kusini.

Akiuzngumza baada ya mchezo huo kumalizika, Dube ambaye ni raia wa Zimbabwe alisema; “Nimefunga lile bao kwenye eneo gumu sana, ukiwa kama mshambuliaji, kwenye angle ile mabeki wengi huwa wanaamini mshambuliaji hawezi kupiga, kwa hiyo unafanya kuwachukua kwenye sapraizi.

"Ninawashukuru viongozi na benchi la ufundi kwa kunileta hapa, ninawashukuru wachezaji wenzangu pia kwa sapoti ambayo wananipa, kazi yetu ni kuwapambania mashabiki zetu wapate furaha. Kwa sasa muunganiko wa timu unaanza kuja, tunaamini mambo mengi yatakuja na tutawafurahisha Wananchi.

“Kuna watu wananisema vibaya lakini Wananchi wananisapoti sana tangu siku ya kwanza, nikivaa hii jezi (ya Yanga) nitapambana sana kwa ajili yao, ninawaambia Wananchi waje Agosti 4 pale kwa Mkapa kwenye siku ya Mwananchi tufurahi sote,” amesema Dube.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: