Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yamaliza utata, Yanga CBE kupigwa Dodoma

Pacome Ewewe CAF yamaliza utata, Yanga CBE kupigwa Dodoma

Tue, 3 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama wewe ni shabiki wa Yanga ambaye popote ilipo timu hiyo nawe unakuwepo, basi anza kujipanga mapema kwa safari ya kuvuka Bahari ya Hindi hadi Zanzibar baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kubariki rasmi maombi ya timu hiyo kurudiana na CBE ya Ethiopia visiwani humo.

Mara baada ya kujua itavaana na Wahabeshi wakianzia kwanza ugenini kabla ya kurudiana nao baadaye mwezi huu, mabosi wa Yanga fasta walituma maombi CAF wakiomba mchezo huo dhidi ya CBE ukapigwe kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kati ya Septemba 20-22.

Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) limetoa ufafanuzi kwamba New Amaan umepata baraka zote za kutumika kwa mechi zote za awali za michuano hiyo ya Afrika kwa ngazi ya klabu hivyo kila kitu kimekaa sawa na Yanga itaenda Zenji kurudiana na Wahabeshi na mshindi wa jumla atatinga makundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: