Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga watafanya vizuri kimataifa kuliko Simba - Mchambuzi

Yanga Mazoezi DA Yanga watafanya vizuri kimataifa kuliko Simba - Mchambuzi

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia runinga ya TV3, Boiboi Mkali, amesema kuwa Klabu ya Yanga wana uwezo wa kufanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika kuliko wapinzani wao SImba SC.

Boiboi amesema hayo ikiwa ni siku chache zimesalia kabla ya Yanga kuwavaa Al-Merrikh ya Sudan wakati Simba wakiwavaa Power Dynamos ya nchini Zambia, ambapo mechi zote zitapigwa Jumamosi, Septemba 16, 2023.

"Huu ni msimu ambao Yanga inaweza kufanya vizuri zaidi kuliko Simba kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa sababu msimu huu Yanga wana wachezaji wengi ambao wanaweza kuamua matokeo ya mechi kuliko msimu uliopita ambapo alikuwa anategemewa mchezaji mmoja tu kufanya maamuzi ya mechi," amesema Boiboi.

Simba imekuwa ikifanya vizuri katika michuano ya Afrika lakini kwa miaka mitano wamekuwa wakiishia kwenye hatua ya robo fainali, wakati kwa upande wa yanga walikuwa wakifanya vibaya lakini msimu uliopita walifanikiwa kufanya vizuri na kufika hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga na Simba zote zimefanya usajili mpya msimu huu lakini wachezaji wa Yanga wanaonekana kutengeneza muunganiko mzuri na hali ya kuelewana wanapokuwa wakitekeleza mbinu za Kocha wao Miguel Gamondi hali inayowafanya kupata matokeo chanya kwenye mechi zao na kuwa tishio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: