Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawili mbaroni kwa uzushi

MASEJOOOOOOOOOOOO Wawili mbaroni kwa uzushi

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii kuhusiana na video ya binti mmoja aliyefanyiwa ukatili hivi karibuni Jijini Dar es Salaam wakidai kuwa amefariki dunia suala ambalo sio kweli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Venance Malya (54) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha na Izack Elias (44) mkazi wa Daraja Mbili Jijini Arusha.

SACP Masejo amebainisha kuwa bado Jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa shauri hilo na pindi utakapokamalika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuepuka kusambaza ama kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandano ya kijamii kwa lengo la kuleta taharuki au kutafuta umaarufu kuacha mara moja kwani ni makosa na wataendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: