Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 10 wafa kwa kufyatuliwa risasi dukani

Ajali Mauaji Mauaji

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wstu 10 wameuawa na watatu kujeruhiwa vibaya baada ya mtu mmoja aliyevalia mavazi ya kijeshi kuingia katika duka kubwa huko Buffalo, jiji la pili kwa ukubwa katika jimbo la New York na kuanza kufyatua risisi hovyo zikilenga wanunuzi.

Kamishna wa polisi wa Buffalo amedai mshambuliaji huyo alikuwa akirusha mbashara ufyatuaji wa risasi kwenye jukwaa la Twitch. Picha kadhaa zilizochukuliwa kutoka kwenye mtandao huo zinaonesha mwili ukiwa umelala sakafuni na mwanamke akipigwa risasi kichwani.

"Ni kama kutembea kwenye sinema ya kutisha, lakini kila kitu ni halisi," afisa wa polisi katika eneo la tukio alinukuliwa akisema na Buffalo News.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: