Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakamatwa kwa mauaji ya bodaboda

Kaster Ngonyani (14).jpeg Wakamatwa kwa mauaji ya bodaboda

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kosa la mauaji ya dereva bodaboda aliyekutwa ameuawa Julai 24 katika Kijiji cha Stalike wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani, amesema baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilianza kufanya msako na hatimaye kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodaboda mkoa wa Katavi Issack Daniel, amewaasa bodaboda kutokuwa na tamaa ya fedha pindi wanapotiliamashaka mienendo ya wateja wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: