Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waichapa Prisons Uwanja wa Sokoine

Simba Vs Prisons 1 0.jpeg Simba waichapa Prisons Uwanja wa Sokoine

Tue, 22 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Bao pekee la Simba SC leo limefungwa na beki Mcameroon, Che Fondoh Malone Junior dakika ya tano tu ya mchezo akimalizia mpira uliomponyoka kipa kipa Adam Mbise kufuatia shuti la mpira wa adhabu la kiungo Kibu Denis Prosper.

Kwa ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya pili, nyuma Singida Black Stars yenye pointi 19 baada ya wote kucheza mechi saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: