Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wadondosha alama mbele ya Coastal Ligi Kuu

Simba Vs Coastal UN Simba wadondosha alama mbele ya Coastal Ligi Kuu

Fri, 4 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vigogo, Simba SC wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Coastal Union ya Tanga leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.

Simba waliuanza vizuri mchezo huo na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza 2-0 kwa mabao ya beki na Nahodha wake, Mohamed Hussein 'Tshabalala' dakika ya 25 na mshambuliaji wake mpya, Mcameroon Christian Leonel Ateba Mbida kwa penalti dakika ya 40.

Coastal Union walirejea na mipango mipya kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa winga wake Mkenya, Hassan Abdallah Hassan dakika ya 47 na beki wa kushoto, Mkongo Hernest Briyock Malonga dakika ya 71.

Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 13 katika mchezo wa tano, wakati Coastal Union inatimiza pointi tano katika mchezo wa saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: