Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Yanga yapata mserereko Klabu Bingwa, Mechi zote kupigwa Dar

Yanga Vs Augusburg Rasmi: Yanga yapata mserereko Klabu Bingwa, Mechi zote kupigwa Dar

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Vital’O ya Burundi imehamishia mechi yao ya nyumbani wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Chamazi Complex. Hii ni kutokana na Burundi kukosa uwanja ulioidhinishwa kwa ajili ya mechi za CAF.

Mabingwa wa hao wa Ligi Kuu bara msimu uliopita wamepangwa kuvaana na Vital’O FC ya Burundi kwenye mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo Yanga itaanzia ugenini lakini itacheza mechi zote mbili ndani ya ardhi ya Tanzania.

Mchezo wa mkondo wa kwanza unatarajiwa kupigwa Agosti 16-18 katika dimba la Benjamin Mkapa huku mkondo wa pili ukipigwa Agosti 23-25 mwaka huu katika dimba la Azam Complex, Chamazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: