Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramli chonganishi inavyopukutisha watu Moro, RPC afunguka

Musilimu 1 RPC Forfunatus Musilimu

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi mkoani Morogoro inawashirikia watu wanane kwa tuhuma za mauaji na kujihusisha kupiga ramli chonganishi ambazo kwa kiwango kikubwa zimechangia kuleta migogoro na mtafaruku katika jamii.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilimu amesema kwenye mdahalo wa Wadau wa Habari juu ya Ulinzi na Usalama wa Mwandishi wa Habari mkoa wa Morogoro uliandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari wa mkoa wa Morogoro (MOROPC).

Mdahalo huo ulifanyika chini ya ufadhili wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushiriniana na International Media Support (IMS).

Musilim amesema kufuatia wimbi la mauaji yaliyojitokeza na utekelezaji wa oparesheni ya kuzuia mauaji ya watu wasio na hatia, tayari watu wawili wametiwa mbaroni kwa tuhuma wakijihusisha upigaji ramli chonganishi kwenye jamii.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo amesema katika kipindi hiki watuhumiwa sita wamekamatwa wakihusishwa na matukio ya mauaji na wanaendelea kuhojiwa zaidi kwa ajili ya utaratibu wa kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Amesema katika kukabiliana na mauaji ya aina hiyo ametenga siku ya Alhamisi ya kila wiki kwa ajili ya kuonana na wananchi wenye migogoro , mitafaruku katika familia na kwenye jamii.

“Kwa sababu tumebaini katika mauaji haya yanayoendelea sehemu mbalimbali za nchi yamekuwa na vyanzo vyake na zaidi yanatoka katika jamii, katika familia au jamii kwa jamii , unaanza ugomvi wa kutoelewana ndani ya familia,” anasema Musilim.

Amesema wananchi wa mkoa huo watakuwa wakifika ofisini kwake kwa ajili ya kuelezea migogoro iliyopo na kuona namna ngani kwa pamoja wataweza kuitanzua hiyo migogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: