Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwalimu Auawa kwa Kupigwa na Kitu Kizito

Mwalimu Auawa Mwalimu Auawa kwa Kupigwa na Kitu Kizito

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWALIMU wa Shule ya Msingi Kisokwe, Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma Albert Kaguli (43) amekutwa ameuawa na watu wasio julikana kwa kupigwa kichwani na kitu kinachosadikiwa kuwa kizito.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP)Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini aliyefanya uhalifu huo.

Aidha amesema jeshi hilo pia linamtafuta mtu mmoja anaye julikana kwa jina la Shukuran Maselo Kwa uchunguzi zaidi kwa kushukiwa kushiriki katika mauaji hayo ambayo chanzo chake inadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kutokana na tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Josephat Maganga amelaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: