Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Musonda aiwahi Singida Fountain Gate

Yanga Musonda010 Musonda aiwahi Singida Fountain Gate

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutokuonekana kwenye mchezo dhidi ya Azam kutokana na majeraha, beki kisiki wa Yanga Yao Kouassi pamoja na mshambuliaji Kennedy Musonda wamerejea.

Yanga inajiandaa kuvaana na Singida Big Stars mchezo utakaopigwa Ijumaa hii Uwanja wa Mkapa.

Musonda amekosekana kwenye mechi tatu mfululizo dhidi ya Ihefu FC, Geita Gold na Azam FC kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi amethibitisha ufiti wa mshambuliaji huyo.

Wakati Musonda akirejea beki kisiki wa timu hiyo Yao amerudi kwenye uwanja wa mazoezi baada ya jeraha lake dogo alilolipata mazoezini kupona na hivyo ni uhuru wa kocha kama ataamua kumtumia kwenye mchezo dhidi ya Singida au hapana.

“Yao amehusika kwenye mabao mengi ya timu pia Musonda amefunga hivyo kurudi kwao wataongeza nguvu na kasi kutokana na kuwa na nguvu walizozitunza baada ya kukosekana kwenye michezo kadhaa.” alisema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: