Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtuhumiwa mauaji ya dada wa bilionea Msuya "Nateseka gerezani, kosa silijui"

Msuya Msdf Mtuhumiwa mauaji ya dada wa bilionea Msuya "Nateseka gerezani, kosa silijui"

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara Revocatus Muyela anayetuhumiwa kumuua dada wa marehemu Erasto Msuya maarufu kwa jina la Bilionea Msuya, Aneth Msuya amesema anateseka gerezani kwa kosa ambalo halijui.

Muyela na aliyekuwa mke wa Bilionea Msuya Miriam Mrita wanatuhumiwa Mei 25, 2016 walimuuwa, Aneth Msuya nyumbani kwake, Kibada Kigamboni , jijini Dar es Salaam.

Mshitakiwa huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akiwa chini ya ulinzi wa askari Magereza wakati akisindikizwa kupanda basi kurudi mahabusu Segerea, baada ya kesi yao kuahirisha.

“Waandishi wa habari mnaona yanayoendelea mahakamani, nateseka kwa kosa ambalo silijui ila Mungu atasimama mimi ni Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM),” alisema Muyela.

Muyela alisema hayo kutokana na ubishani wa kisheria uliyokuwa umetokea ndani ya chumba cha mahakama kuhusiana na taarifa ya awali ya siri ya Jeshi la Polisi (First crime report) ya tukio hilo la mauji.

Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Jaji Edwin Kakolaki wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo leo Shahidi wa 23, Sajenti Obadia Mwarukuta ataendelea kuulizwa maswali ya dodoso na Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala na Nehemiah Nkoko.

Sajenti Mwarukuta katika ushahidi wake alieleza utofauti wa vielelezo vya mahakama kilicholetwa na upande wa utetezi na upande wa Jamhuri ambavyo vyoye vilikuwa ni taarifa ya siri ya jeshi hilo ya tukio moja.

Shahidi huyo ambae ni Ofisa wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Dodoma, alidai kuwa taarifa hizo zinautofauti kwa sababu ya upande wa utetezi ni nakala na ya Jamhuri ni halisi (original) na ndiyo ambayo ilikuwa inatembea mara kwa mara ndani ya jeshi hilo.

Alidai kuwa mwaka 2016 alikuwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Dar es Salaam Kitengo cha Kumbukumbu cha Makosa ya Jinai na kwa sasa yupo Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya mkoani Dodoma.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Paul Kimweri, Sajenti Mwarukuta alidai kuwa Mei 30,2016 aliingia kazini, wakati anaendelea na kazi zake zingine alizopangiwa kuna nyaraka alizipokea kutoka mkoa wa kipolisi Temeke zinazohusiana na jinai.

“Hizi nyaraka mbili nikizingalia DE III ni nakala na hii PE 17 ni nyaraka halisi, kwa uhalisia hazifanani. Nikiangalia eneo la juu ya hizi nyaraka kuna utofauti kwa jinsi zilivyojazwa,” alidai Sajenti Mwarukuta.

Shahidi aliendelea kudai kuwa kielelezo PE 17 kwenye namba ya upelelezi ya RCO ilipoandikwa ipo chini ya neno confidential (siri), ndipo linapotakiwa iandikwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: