Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke amuua mumewe kwa kumchoma kisu tumboni

Kisuuu 80 Mke amuua mumewe kwa kumchoma kisu tumboni

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Fadhila Balama mkazi wa Mtaa wa Kitwiru A, Manispaa na wa Mkoani Iringa anatuhumiwa kumchoma na kitu chenye ncha kali mume wake Denis Chumbula hadi kupelekea kifo baada ya kuibuka mzozo baina yao.

Mwenyekiti wa Mtaa huo, Nazareno Mangw'ata amesema tukio hilo limetokea usiku wa Jumatatu ya Novemba 27, 2023 na kwamba mwanamke huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kufuatia tuhuma za kusababisha mauaji hayo.

Mangw'ata ameongeza kuwa familia hiyo imekuwa na ugomvi wa mara kwa mara huku mwanamke huyo akituhumiwa kumpiga mume wake kwa kutumia fimbo na wakati mwingine vitu mbalimbali ikiwamo kumpiga na tofali.

Upande wake Diwani wa Kata ya Kitwiru, Dkt. Hamza Mwanuhehe akizungumzia tukio hilo ametoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya ukatili na kuhimiza wanafamilia wanapogombana kutumia njia sahihi kupata suluhu.

Mjomba wa marehemu Denis Chumbula aitwaye Victor Kihaga amesema alipokea taarifa za mpwa wake kuchomwa na kitu chenye ncha kali kutoka kwa majirani na baada ya kufika alikuta marehemu anavuja damu nyingi tumboni.

Kwenye mazungumzo yake marehemu alimweleza mjomba wake kuwa ugomvi wao ulitokana na mke wake kuchelewa kurudi nyumbani na alipumuuliza alitoa kauli mbaya na ndipo alipompiga kofi.

Baada ya kumpiga kofi mke wake alienda kuchukua Kisu na kuanza kumchoma maeneo ya tumboni, mjomba alishirikiana na majirani kumpeleka Hospitali Mpwa wake lakini alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: