Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauaji yamsikitisha Anna Makinda

Mauaji Mwanza Mauaji yamsikitisha Anna Makinda

Fri, 4 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda amesema anasikitishwa na vitendo vya matukio ya mauaji vinavyoripotiwa maeneo mbalimbali nchini.

"Tanzania hakuna ukabila kwa sasa, tumechanganyika sana, hakuna familia ambayo ni kabila moja, lakini bado matukio ya mauaji yanaendelea inasikitisha sana, tumekosea wapi jamani, turudini kwa Mwenyezi Mungu"

“Nimeona kwenye taarifa ya habari, baba kamuua mtoto wake wa miezi mitatu, mtoto kakosea nini? Siku za karibuni mauji yamekuwa ni mengi na yanashamiri na kuzoeleka kama kitu cha kawaida, viongozi wa dini tusaidieni hili,” amesema Spika Mstaafu Anna Makinda wakati wa maadhimisho ya Jumuiya ya Maridhiano Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: