Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauaji ya Swalha, rafiki wa muuaji asimulia mazito

Rafiki Wa Said Mauaji ya Swalha, rafiki wa muuaji asimulia mazito

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bado ni mwendelezo wa taarifa ya simanzi kwa familia ya Swalha kufuatia tukio la mauaji ya mwanamke huyo ambaye alikuwa akijishughulisha na masuala ya urembo (make-up artist) kuuawa na mumewe aliyetambulika kwa jina la Said linazidi kuibua mambo mengi na mzito.

Usiku wa kuamkia jana Jumapili Mei 29, 2022 Swalha alidaiwa kuuawa na Said Oswayo kwa kupigwa risasi 7 za kichwani nyumbani kwao, Buswelu jijini Mwanza. Taarifa kutoka kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa chanzo ni wivu wa kimapenzi.

Rafiki wa mtuhumiwa (Said) aitwaye, Chamagenge John Kilosa anasimulia; “Watoto wangu (akiwemo Swalha) waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

Said Oswayo ni ni rafiki yangu kwa miaka Zaidi ya 20, tumefanya naye kazi kwa muda mrefu. Hata mkewe wa kwanza, Mama Ashirafu ni shemeji yangu, kwani ni mdogo wake na mke wangu. Ni mtu ambaye tumekuwa naye karibu kwa siku nyingi.

Taarifa za tukio hilo nilizipata saa 7 usiku, kuna mtu alinipigia simu akanipa taarifa hizo wakati nikitoka kwenye mpira wa Real Madrid na Liverpool.

Akaniambia amempiga risasi mkewe na kumuua nay eye amekwenda kujiua. Baada ya hapo, nilianza kupokea simu nyingi kwa sababu ndugu walijua niko karibu naye hivyo pengine nafahamu, mimi niliwaeleza taarifa za awali kama nilivyozipokea, hivyo sina taarifa nyingine wala siwezi kuhakikisha kama ni kweli limetokea.

Ikabidi nizime simu, nijipe muda wa kutafakari nini kimetokea, nikaamka saa 11 alfajiri nikaja mpaka nyumbani kule Buswelu kwa Said, nikakuta nyumba imefungwa. Nikauliza majirani wakasema kweli tukio limetokea na mtoto (Ashirafu, mtoto wa mume) amepelekwa kwao na marehemu.

Ikabidi nije msibani, nikawasiliana na shemeji ambaye ni mdogo wa marehemu, akaniambia kuna taarifa zinahitajika polisi, tukaenda kule. Askari wakachagua ndugu wachache tukaingia ndani kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Jamaa alikuwa anampenda sana mke wake na mke wake alikuwa anampenda sana mumewe, sikuwahi kusikia kama kuna tatizo, hata mara ya mwisho tunapotezana walikuwa vizuri tu mpaka nilipokuja kusikia amefanya tukio kama hilo sikuamini, ilinishitua na nikataka kujua kuna nini?

Kwa taarifa za mdogo wa marehemu, jamaa alikuwa amesafiri na mke hakuwepo nyumbani, hivyo mwanaume alivyorudi akampigia simu mkewe arejee nyumbani kwani alikuwa amechoka, inavyoonekana mke alichelewa kurudi nyumbani labda kwa sababu mbili tatu, ndio ikasababisha ugomvi.

Kuhusu taarifa za alipo Said sina, kwakweli sijui yuko wapi na yuko katika hali gani,” amesema Chamagenge.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: