Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu! Kaburi lakutwa na nazi, mayai vinza

Nazi Mayai Vinzaaa Maajabu! Kaburi lakutwa na nazi, mayai vinza

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Mtaa wa Mafuriko, iliyopo Kata ya Mzizima Mkoani Tanga wamepata taharuki baada ya kusambaa kwa taarifa za uwepo wa kaburi la Mwanamke mmoja mwenye asili ya kiarabu aliyeuawa na kuzikwa kwenye eneo la Mwekezaji kitendo kilichopelekea Serikali kuamua kufukua kaburi hilo ili kujiridhisha.

Akiongea baada ya zoezi la uchimbaji wa kaburi hilo Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amesema Mara baada ya kupata taarifa walichukua hatua za kufukua kaburi hilo kwa kibali cha Mahakama ambapo baada ya kufukua kaburi wamekuta mambo ya imani za kishirikina ikiwemo kukutana na sanda nyeusi, nazi tatu na yai viza.

DC Kaji amepiga marufuku Mwananchi yeyote kuonekana katika eneo hilo la Mwekezaji akisema kumekuwa na tabia ya Wananchi kuvamia maeneo ya wazi na baadaye kuomba fidia kwa Serikali jambo ambalo linapelekea matatizo makubwa ya migogoro ya ardhi ambayo mara nyingi ni uvamizi wa Wananchi kwenye maeneo yenye hati miliki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: