Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatutovumilia sheria zilizopigwa marufuku na FIFA - Polisi

Muliro Jumanne Marufuku Hatutovumilia sheria zilizopigwa marufuku na FIFA - Polisi

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limejipanga vizuri kuhakikisha Ulinzi na Usalama unakuwa wa Uhakika wakati wa Ufunguzi wa shindano la African Football League, kesho Ijumaa ya oktoba 20, 2023 wakati Simba SC itacheza na Al Ahly SC ya Misri kwenye dimba la Mkapa.

Taarifa hiyo imetolewa Jumatano ya leo Oktoba 18, 2023 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro ambayo amepiga marufuku mashabiki kufanya vurugu wakati wa Kuingia Uwanjani ili kuhepuka usumbufu.

Kamanda Muliro ameendelea kwa kusema, Jeshi la Polisi halitovumilia tabia zozote zile zilizopigwa marufuku na FIFA, CAF na TFF ambazo zinaweza kupelekea Tanzania kukosa sifa ya kuandaa mashindano kama haya wakati mwingine kwani watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa Upande Mwingine Kuelekea kwenye mchezo huo, Mashabiki wa Simba SC na Katibu wa matawi Simba SC Jijini Mwanza, wameelezea tambo zao za kupata ushindi dhidi ya Al Ahly utakaochezwa saa 12:00 Jioni Ijumaa Oktoba 20, 2023 kwenye dimba la Mkapa, Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: