Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Apata kifafa akivua samaki baharini na afariki dunia

ACP Nicodemus Katembo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo.

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Mnete, Said Ally (24) amefariki duniani wakati akivua samaki pwani ya bahari katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa Oktoba 17, 2023 mtu huyo alikutwa akiwa amekufa maji wakati akivua samaki baharini.

Amesema kuwa mtu huyo aligunduliwa kuwa amefariki majira ya saa nne asubuhi, huku chanzo cha kifo chake kikiwa ni kuzama kwenye maji wakati akivua samaki. Hata hivyo uchunguzi wa daktari umebaini kuwa marehemu amefariki kwa kukosa hewa baada ya kuzama kwenye maji.

“Jamii ya wavuvi inayofanya shughuli za uvuvi inapaswa ichukue tahadhari za kiusalaama pindi wanapoenda bahari  ili kuepuka ajali zinazoweza kutokea wanapokuwa baharini wakivua samaki,” amesema Katembo.

Shomari Ismail baba mkubwa wa marehemu amesema kuwa marehemu alikuwa na ugonjwa kudondoka yaani kifafa hata uvuvi wake ulikuwa wa maji madogo.

“Unajua marehemu alikuwa na ugonjwa wa kudondoka kifafa ambapo kifafa kilimtokea akiwa baharini ambapo alienda kuvua na huwa anaena mara kwa mara kuvua kando kando mwa bahari kutokana na tatizo lake hakuwa anatumia mtumbwi halafu familia haikujua kama amekwenda huko,” amesema Ismail.

Jirani Ismail Chande amesema kuwa marehemu alikuwa na kawaida ya kusubiri maji yajae saa nane mchana ndipo anakwenda kuvua samaki.

“Hata jana alikwenda saa nane mchana kuvua samaki pembezoni lakini kumbe hakurudi nyumbani. Nikiwa dukani nakaribia kufungua duka nasikia msikitini wakitangaza juu ya kifo chake kuwa alifariki baharini hata uvuvi wake haukuwa wa mtumbwi,” amesema Chande.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: