Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuua mkewe kwa risasi 7 naye ajiua, mwili wakutwa Ziwani

Saidi Na Mkewe Swalha Said na mkewe enzi za uhai wao

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume anayefahamika kwa jina la Said Oswayo anayedaiwa kumuua mkewe, Swalha Salum (28) kwa kumpiga risasi amekutwa amejiua kwa kujipiga risasi.

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kupitia kwa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Said amekutwa amejipiga risasi na mwili wake umekutwa ndani ya maji ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza.

"Mwili huo umeopolewa ziwani eneo la ufukwe wa Rock Beach ukiwa na majeraha ya risasi kichwani. Tumejiridhisha kuwa ndiye mtuhumiwa baada ya kutambuliwa na ndugu zake," amesema Kaimu Kamanda huyo.

Amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake.

Said anadaiwa kumuua mkewe, Swalha tukio lililotokea katika nyumba yao maeneo ya Buswelu Mwanza, juzi Jumamosi, Mei 28, 2022 kufuatia ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi baina ya wanandoa hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: