Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajiua Kisa Kuachwa na Mkewe

MWAIBAMBE WEB.jpeg Ajiua Kisa Kuachwa na Mkewe

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linaendelea kuchunguza tukio la kijana aitwaye Ginasa Petro (30) Mkazi wa Bariadi aliyekunywa sumu ya kuulia panya akiwa Wilayani Nyang'hwale na kupoteza maisha huku chanzo cha kujiua kikiwa ni msongo wa mawazo baada ya kuachwa na mkewe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha kifo hicho kinatokana na mgogoro wa kifamilia ambapo Mke wa Ginasa aitwaye Sara Jeremia aliondoka nyumbani na kurudi kijijini kwao na kumuacha Ginasa akiwa peke yake.

"Sara Jeremia aliondoka nyumbani walikokuwa wanaishi huko Kakola Shinyanga na kurudi nyumbani kwao kijiji cha Igula ambako alimuacha Mumewe pekee yake hapo nyumbani, Mwanaume huyo alimfuata Mke wake ili arudi nyumbani waendelee kuishi lakini Mke alikataa ndipo Ginasa aliporudi nyumbani na kuchukua maamuzi ya kujiua."

"Mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Daktari na kukabidhiwa kwa Ndugu zake kwa ajili ya mazishi"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: