Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT-Wazalendo yataka uchunguzi kijana anayedaiwa kuuawa Kakonko

Zitto Kabwe ACT Wazalendo yataka uchunguzi kijana anayedaiwa kuuawa Kakonko

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT Wazalendo, kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillius Wambura, kuunda tume ya makamishna wa jeshi hilo kwa ajili ya kuchunguza kifo cha utata cha mfanyabiashara Enock Elias, Mkazi wa Kijiji cha Ilabiro Kata ya Katanga, Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Enock Elias anadaiwa kuuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa kwenye mikono ya polisi na maafisa wa idara ya uahamiaji wilayani Kakonko.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwenge wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema hatua hiyo itasaidia familia ya kijana huyo kupata haki na kujua chanzo cha kifo chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: