Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zakazakazi: Azam tumepata hasara

Azam Official Team Zakazakazi: Azam tumepata hasara

Fri, 5 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria maarufu kama Zakazakazi amedai kuwa klabu yao imepata hasara baada ya mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba Sc kusogezwa mbele.

Kauli hiyo ya Zakazakazi imekuja baada ya TFF kuisogeza mbele mechi hiyo kutoka Mei 6, 2023 hadi Jumapili Mei 7, 2023.

"Tumepata athari ya kifedha baada ya mchezo (dhidi ya Simba Sc) kusogezwa mbele, kwa sababu mchezo kama ungechezwa tarehe 6 kama ilivyopangwa basi tarehe 7 tungerudi na hivyo watu wangepumzika na kusingekuwa na haja ya watu kukaa kambini kuwahudumia.

"Lakini wametuongezea siku moja mbele ambayo sisi haikuwepo kwenye ratiba, hivyo muda wa maandalizi na kukaa kambini umeongezeka, na hivyo tumepata hasara kutokana na kuwahudumia watu siku hiyo wakiwa kambini" amesema Zakazakazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: