Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenyeji Cameroon wafuzu robo fainali, AFCON

Cameroon Robo Final Cameroon yafuzu Robo fainali AFCON

Tue, 25 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji wa michuano ya soka ya mataifa barani Afrika AFCON timu ya taifa ya Cameroon imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa 16 bora dhidi ya timu ya taifa ya Comoro. Na wataminyana na Gambia kwenye mchezo wa robo fainali.

Mabao ya Cameroon yamefunga na Karl Etoko Ekambi dakika ya 29 na Vincent Abubakar alifunga dakika ya 70 na bao pekee la Comoro limefungwa na Mchangama dakika ya 81.

Ushindi huu umeifanya Cameroon ambao ndio wenyeji kufuzu hatua ya robo fainali ambapo watacheza dhidi ya timu ya taifa ya Gambia ambao wamefuzu robo fainali kwa mara ya kwanza wakiwa wanashiriki michuano hii baada ya kuifunga Guinea bao 1-0, bao pekee la Mussa Barrow dakika ya 71.

Kivutio kikubwa kwenye mchezo wa Cameroon na Comoro ilikuwa ni kiwango walichoonyesha timu ya taifa ya Comoro ambao wameshiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano hii walitoa upinzani mkubwa sanaa dhidi ya wenyeji. Comoro Waliingia kwenye mchezo wa usiku wa jana wakiwakosa magolikipa wao wote 3 kwa sababu ya majeruhi na maambukizi ya Uviko 19 na iliwalazimu kumtumia beki Chaker Alhadhur kama golikipa kwenye mchezo huo na dakika ya 7 ya mchezo wakapata pigo baada ya nahodha wao Nadjim Abdou kuonyeshwa kadi nyekundu.

Michezo ya hatua ya 16 bora inaendela tena leo kwa michezo miwili Senegal wanacheza dhidi ya Cape Verde na Morocco wanaminyana na Malawi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: