Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wazungu acheni dharau kwa AFCON - Haller

Sebastian Haller Sebastian Haller.

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Sébastien Romain Teddy Haller raia wa Ivory Coast amewatolea uvivu wazungu kwa kuibeza michuano ya Ligi ya Mataifa Afrika (AFCON) baada ya kuulizwa swali la kizushi na mwandishi kuhusu uwezekano wa yeye kwenda Afrika kushiriki michuano hiyo.

Sébastien Haller (29) ambaye alizaliwa Ufaransa na amewahi kucheza kwenye timu ya vijana ya Ufaransa kabla ya kugeukia nyumbani kwao Ivory Coast amechagua kucheza AFCON hasa ikizingatiwa kuwa timu yake imefuzu michuano hiyo.

Mtangazaji kuelekea AFCON 2022: "Je, ungependa kusalia katika klabu yako Januari au kucheza AFCON?"

Sebastian Haller: "Swali hili linaonyesha ukosefu wa heshima ulionao kwa Afrika. Je, unaweza kumuuliza swali hili mchezaji wa Ulaya kuelekea michuano ya EURO? Bila shaka nitacheza AFCON."

Ikumbukwe kuwa, wachezaji 43 Waafrika wanaokipiga katika Ligi Kuu ya Uingereza watarejea Afrtika kwa ajili ya michuano hiyo huku Nottingham Forest FC ikitarajiwa kuondokewa na nyota wake 8 wa kikosi cha kwanza watakaoshirikishi michuano hiyo mikubwa Barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: