Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu nane wafariki katika mkanyagano AFCON

Vifo Mashabiki Cameroon Baadhi ya Mashabiki wakisaidia majeruhi katika tukio hilo la kukanyagana

Tue, 25 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu nane wamefariki dunia siku ya Jumatatu, katika tukio la mkanyagano nje ya uwanja ambako Cameroon ilikuwa inacheza dhidi ya Comoro, katika mechi ya kufuzu robo fainali ambayo Cameroon imeshinda kwa magoli 2-1.

Wenyeji wa michuano hiyo Cameroon wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya Comoro, katika mechi iliyoshuhudia vifo vya watu wasiopungua wanane na wengine kadhaa wakijeruhiwa katika mgandamizo nje ya uwanja wa Olembe mjini Yaounde, ambako mechi hiyo ilichezwa.

Gavana wa mkoa wa Kati wa Cameroon, Naseri Paul Biya, amesema huenda kukawa na vifo zaidi. Maafisa katika hospitali ya karibu ya Massassi wamesema wamepokea majeruhi wasiopungua 40, waiokimbizwa hospitali hapo na polisi na raia. Maafisa hao wamesema hospitali hiyo haikuwa na uwezo wa kuwatibu.

Mashuhudua waliokuwepo uwanjani wamesema watoto walikuwa miongoni mwa waliokumbwa na mkasa, ambao ulitokea baada ya wasimamizi wa uwanja kufunga milango na kusitisha kuwaruhusu watu kuingia. Maafisa wa soka wamsema karibu watu 50,000 walikwenda kushuhudia mechi hiyo mechi hiyo.

Uwanja huo una uwezo wa kubeba watazamanaji 60,000 lakini haukupaswa kuja kwa zaidi ya asilimia 80 kutokana na hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona. Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF, linaloendesha michuano ya kombe la Afrika, limesema linafahamu juu ya tukio hilo.

Mmoja ya maafisa wa juu wa shirikisho hilo, katibu mkuu Veron Mosengo-Omba, alikwenda kuwatembelea mashabiki waliojeruhiwa hospitalini, imesema CAF katika taarifa na kuongeza kuwa inafanya uchunguzi kubaini hasa chanzo cha mkanyagano huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: