Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upelelezi kesi ya aliyekua kocha Simba badobado

Mwarami Ooo Aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Muharami Sultani

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Upande wa mashtaka katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Muharami Sultan (40) na wenzake umedai kuwa bado unaendelea na upelelezi wa shauri hilo.

Sultan na wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo ya kusafirisha dawa hizo zenye uzito wa kilo 34.89 pamoja na kutakatisha fedha.

Wakili wa Serikali, Frank Rimoy aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Hata hivyo, Agosti 5, 2024 Mahakama hiyo iliupa mwezi mmoja upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi baada kudai upo hatua za mwisho kukamilisha shauri hilo.

Rimoy alitoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.

Baada ya kueleza hayo, wakili wa washtakiwa Razaq Wanga alidai hana cha kueleza na wanasubiri tarehe nyingine kujua upelelezi kama umekamilika, kisha Hakimu Lyamuya aliahirisha kesi hadi Septemba 2, 2024 kwa ajili ya kutajwa. Shauri hilo limesikilizwa kwa video washtakiwa wakiwa rumande.

Mbali na Sultan, washtakiwa wengine ni mmiliki wa Kituo cha Cambiasso Sport Academy, Kambi Zubery Seif; Said Matwiko mkazi Magole na Maulid Mzungu maarufu Mbonde mkazi wa Kisemvule ambaye ana undugu na mtuhumiwa Muharami. Wengine ni John John mkazi wa Kitunda na Sarah Joseph. Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka manane likiwemo la kuongoza genge la uhalifu shtaka linalowakabiliwa wote ambapo inadaiwa tarehe tofauti kati ya mwaka 2016 na Novemba 4, 2022 maeneo tofauti ya Dar es Salaam na Pwani washtakiwa waliongoza kwa lengo la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Shtaka la pili inadaiwa kuwa Oktoba 27, 2022 katika eneo la Kivule Wilaya ya Ilala kwa pamoja walikutwa wakisafirisha dawa hizo zenye uzito wa kilo 27.10.

Vilevile, Novemba 4, 2023 Zuberi, Zungu na Mtwiko katika eneo la Kamegele Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, walikutwa wakisafirisha Heroin zenye uzito wa Kilo 7.79. Katika shtaka la nne, tano, sita na saba ambayo ni ya utakatishaji fedha yanayomkabili Kambi inadaiwa Aprili 15, 2021 katika wilayani Ilala alinunua magari manne aina ya TATA yenye jina la Safia Group of Companies Ltd huku akijua mali hizo zilipatikana kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu.

Katika shtaka la nane inadaiwa Aprili 20, 2021 Kambi alinunua gari aina ya TATA yenye jina Safia Group of Companies Ltd akijua mali hiyo ilipatikana kwa kosa la kuongoza genge la uhalifu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: