Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujerumani yatinga 16 Bora EURO 2024

IMG 0782.jpeg Ujerumani yatinga 16 Bora EURO 2024

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WENYEJI, Ujerumani wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2024 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hungary katika mchezo wa Kundi A usiku wa Jumatano Uwanja wa MHPArena Jijini Stuttgart.

Pongezi kwa wafungaji wa mabao ya ‘Nationalelf’, viungo wa Bayern Munich mwenye asili ya Nigeria, Jamal Musiala dakika ya 22 na İlkay Gündoğan wa Barcelona mwenye asili ya Uturuki dakika ya 67.

Kwa ushindi huo, Ujerumani wanafikisha pointi sita pamoja na ushindi wa mechi ya kwanza wa 5-1 dhidi ya Scotland na wanajihakikishia kusonga mbele kwa sababu timu pekee yenye uwezo wa kuzikatama pointi hizo ni Uswisi pekee baada ya sare ya 1-1 na Scotland usiku wa Jumatano.

Nayo Croatia imetoka sare ya 2-2 na Albania katika mchezo uliotangulia wa Kundi B.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: