Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uchambuzi: Taifa Stars ilifanikiwa hapa kuwaadhibu Guinea

Mzize Mudathir Taifa Stars ilifanikiwa hapa kuwaadhibu Guinea

Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Guinea katika mchezo wa kufuzu fainali za AFCON 2025 nchini Morocco. Magoli pekee ya Stars yakifungwa na Feitoto 61' na Mudathir Yahya 88' wakati la Guinea likufungwa na Mohamed Bayo 57'

Nimeipenda na nimevutiwa na muundo wa uzuiaji wa timu yetu.

1: Kwanza kabisa hakuna spaces kwenye mistari yetu yote mitatu katika 4-4-2

2: Timu ipo "narrow" sana kwamba ni unawaambia Guinea njia pekee labda pembeni lakini hakuna njia ya ndani.

3: Wachezaji wana move kwa pamoja as a unit, hakuna kuachana distance kubwa baina ya mchezaji mmoja na mwingine.

4: Shinda mipira ya pili mingi pamoja na kushinda mipambano yako (win duels and second balls).

Nafikiri bila mpira sidhani kama kuna kingine ambacho kocha na wachezaji wangefanya zaidi ya pale (Yes hakuna kitu kamilifu) lakini kile ndio bora ambacho benchi la ufundi na wachezaji wamefanya.

Kitu pekee ambacho kilikuwa adui wetu mkubwa ni kutoka kwetu pekee ni zile "Turn Overs" kupoteza mipira kirahisi hasa maeneo hatarishi (na ilitokea sana kipindi cha pili kama mara tatu ) na mara moja tukaadhibiwa na Bayo.

Tukiwa na mpira ni sehemu inayofuata ya kuboresha maana leo ilikuwa kucheza na nyakati (Pick our moments) kwamba ikitokea mpira uliokufa, uwezo wa mchezaji mmoja mmoja (Feisal), makosa ya mpinzani (Mudathir ). Wachezaji wawili ambao wamefanya umaliziaji mzuri sana.

Guinea, licha ya kuwa na mpira muda mrefu lakini unaona wanafungaje goli (uzuiaji mzuri wa Stars) lakini sababu nyingine

1: Decision making yao kwenye mita 25 za mwisho, aina ya pasi na movements ilikuwa duni.

2: Touches nyingi kabla ya kuachia pasi haraka

3: Hakuna runners wengi bila mpira asilimia kubwa wanataka mpira mguuni

4: Kwa vimo vyao virefu mipira ya juu bado hawakuwa wafanisi

FAHAMU

1: Wale vitasa vyao viwili miili nyumba ni huruma kwa Waziri Jr

2: Work rate yetu leo hasa bila mpira

3: Nahodha wao pale kati physically alitumudu (ila nilipenda wachezaji wetu hawakuacha kupambana naye).

4: Turn Overs hatari sana kwenye soka, silaha kali

5: Feisal ule mkwaju bila kupata "Backlift"

6: Mudathir huwa ananusa lose balls kama namba 9

7: Walinzi wetu + Golikipa

FT: Guinea 1-2 Taifa Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: