Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Dabo awaangushia lawama wachezaji wapya sare ya JKT Tanzania

Azam Jkt Bilabila Dabo: Wachezaji wapya ndio sababu ya kushinda kuwafunga JKT Tanzania

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Azam SC, Youssouph Dabo amesema kuwa kilichowafanya wakashindwa kupata matokeo mbele ya JKT Tanzania ni kutokana na wachezaji wapya kushindwa kuingia kwenye mfumo wa kocha huyo.

Dabo amesema hayo baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ya Ligi Kuu iliyopigwa katika Dimba la Meja Jenerali Isamhuyo ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana.

“Tunahitaji kutafakari na kupata majawabu hasa kuhusu wachezaji wapya, kwa sababu nadhani wanahitaji kuzoea. Ukitazama mchezo wa leo (jana) nilijaribu kufanya mabadiliko machache ya kimuundo wa timu, wanahitaji kubadilika ili kuisadia timu.

“Msimu uliopita kuna nyakati tulicheza na washambuliaji wawili, lakini baadhi ya wachezaji wetu imekuwa ngumu kuzoea mfumo wetu kwa sababu walikotoka walikuwa wakicheza kama washambuliaji pekee kwa msano Blanco na Sadoun, kwa hiyo ni ngumu kuzoea kile walichokutana nacho Azam.

“Tunahitaji kuendelea kufanyia kazi mapungufu yetu ili kuwa bora kwenye michezo ijayo kwa sababu huu ni mchezo mmoja tu kati ya michezo 30 ya Ligi na huu ndio ni mchezo wa kwanza lakini kuna michezo mingi inakuja.

“Huwezi kusema tutakosa ubingwa, bado kuna mechi kibao na ni mapema sana, hili ni soka, kwenye soka hakuna timu moja inayoshinda kila mchezo, tulipata nafasi za kufunga lakini hatukufunga, lakini kama unaanza kulialia mechi ya kwanza nadhani utakuwa hujui mpira, kwenye maisha hutakiwi kukata tamaa bali kupambana,” amesem Dabo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: