Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala asifia ubora Afcon

Sifiwe Tshabalala  Dsc Sifiwe Tshabalala.

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Sifiwe Tshabalala amesifu mashindano ya Afcon mwaka huu huko Ivory Coast kuwa ni ya aina yake kutokana na ushindani wa timu na uendeshaji wake,

Tshabalala ni miongoni mwa mastaa walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu katika kila nchi kushiriki katika fainali hizo mwaka huu wakiwa kama mabalozi.

Kiungo huyo aliyefunga bao la kwanza katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 alisema kuwa fainali za Afcon mwaka huu zimeiheshimisha Afrika katika uso wa dunia.

"Nilihudhuria sherehe za ufunguzi ambazo zilikuwa za daraja la kidunia katika nyanja zote. Mpangilio, eneo la tukio, mashabiki na soka lenyewe. Kiwango cha soka kimekuwa cha kuvutia mno.

"Nizungumzie pia kiwango bora cha uchezeshaji mechi na mpangilio mkubwa na mzuri wa Caf. Hii kwa mbali ndio Afcon bora ambayo dunia imewahi kuishuhudia," alisema Tshabalala.

 Tshabalala aliyewahi kucheza Afcon mwaka 2006, 2008 na 2018 akiwa na Afrika Kusini alisema ubora wa mashindano hayo mwaka huu umechangia kupatikana kwa matokeo ya kushangaza.

"Ni michuano migumu kwa timu zote. Ubora ni wa hali ya juu. Kumekuwa na matokeo ya kushtua ya zinazoitwa timu ndogo. Zimeibuka na kushangaza. Hili hapana shaka ni shindano la kushtua," alisema Tshabalala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: