Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taifa Stars yaanza AFCON na kichapo, Novatus alimwa kadi nyekundu

IMG 6504.jpeg Mchezo ulimalizika kwa Morocco kushinda bao 3-0

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Tanzania imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi F usiku huu Uwanja wa Uwanja wa Laurent Pokou Jijini San-Pedro, Ivory Coast.

Mabao ya Simba wa Atlasi yamefungwa na beki wa Al-Shabab ya Saudí Arabia, Romain Ghanem Paul Saïss dakika ya 30, kiungo wa Marseille ya Ufaransa, Azzedine Ounahi na mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri dakika ya 80.

Taifa Stars ilimaliza pungufu baada ya kiungo wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine Novatus Dismas Miroshi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: