Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika mpya amchomoa Ayoub, Camara....

Teba Mz Straika mpya amchomoa Ayoub, Camara....

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji Leonel Ateba, uongozi wa Simba umefikia makubaliano ya kumalizana na Ayoub Lakred kwa lengo la kupisha usajili huo.

Ayoub ameitumikia Simba kwa msimu mmoja na kuifanya timu hiyo ikamaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo inaelezwa ameondolewa kwenye mfumo kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyoyapata kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25.

Chanzo cha kuaminikia kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwanaspoti uongozi wa Simba umefanya uamuzi wa kumtoa Ayoub kutokana na kukosekana kwa huduma yake na tayari wamemsajili kipa mwingine.

“Unajua isingekuwa rahisi kuachana na mchezaji wa ndani wakati eneo la kipa lina makipa wawili wa kigeni hivyo uamuzi ni kumtoa kwenye mfumo na tutaendelea kumlipa kama kawaida,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza;

“Ayoub ataendelea kulipwa fedha yake kama kawaida akiwa nje ya uwanja tunamtazamia hadi dirisha dogo ndio kutakuwa na uamuzi wa mwisho.”

Wakati mtoa taarifa huyo wa kwanza akisema hivyo, taarifa zingine zinasema kuwa kipa huyo ameshapewa fedha yake yote hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo.

“Timu imefikia makubaliano ya kuachana na kipa huyo ambaye yupo nje kwa muda akiuguza majeraha yake na tumefanya hivyo kwa lengo la kuendelea kubaki na Freddy Koubalan,” kilisema chanzo hicho;

“Ni kweli tumefanya usajili wa mshambuliaji mpya lakini hatuna uhakika kama ataingia kwenye mfumo haraka ndio maana tumemuacha freddy ambaye wengi walijua ndiye atakaepisha uasajili mpya.”

Yaliyomkuta Ayoub ni sawa na Aubin Kramo ambaye pia aliobndolewa kwenye mfumo wa usajili kutokana na kupata jeraha kwenye uwanja wa mazoezi na nafasi yake ilichukuliwa na Babacar Sarr ambaye pia aliachwa kutokana na kushindwa kuendana na kasi ya timu hiyo.

Mastaa wa Simba wa kigeni waliobaki sasa ni Moussa Camara, Che Malone, Valentine Nouma, Augustine Okajepha, Joshua Mutale, Fabrice Ngoma, Jean Ahoua, Steven Mukwala, Debora Mavambo, Karaboue Chamoe, Freddy na Ateba ambao ni usajili mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: