Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Song akili kuzidiwa na Senegal

Rigobert Song. Rigobert Song.

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Cameroon, Rigobert Song, Afungwa, lazima tukubali kuwajibuka na kusema ukweli kwamba wenzetu Senegal walikuwa vizuri kwenye mechi kutuzidi.

“Senegal walikuwa na nguvu kutuzidi. Wachezaji wao karibu walikuwa kila sehemu ndani ya uwanja. Walistahili kushinda. Kwa upande wetu tuna vijana wengi kwenye timu ya taifa, hivyo huu ni mwanzo wao wa kupata uzoefu.”

Wakati huo huo, kocha wa Senegal, Aliou Cisse alielezea kutosheka na kiwango cha timu yake katika mchezo huo. Miamba hiyo Simba wa Teranga ambao ni mabingwa watetezi, walijihakikisha kutinga hatua ya 16 bora ya fainali hizo za Afcon 2023 baada ya kukusanya pointi sita katika mechi mbili.

Matokeo ya ushindi wa mabao 3-1 uliwafanya kuongoza kundi lao na kutinga raundi ya mtoano.

Nawapongeza wachezaji wangu kwa sababu wamecheza mechi vizuri sana. Waliheshimu maelekezo yangu na ushauri wote niliowapa,” alisema Cisse.

Kuhusu kocha Song bado ana matumaini makubwa ya kuiongoza Cameroon kwenye kutinga raundi inayofuatia ya michuano hiyo. Cameroon yenye pointi moja sasa imebakiza mechi dhidi ya Gambia, ambao hawana pointi yoyote, huku wakiomba Senegal iichapa Guinea yenye pointi nne kwenye mchezo wao wa mwisho, Jumanne. Cisse na Song ni mastaa wa zamani wa mataifa hayo na katika enzi zao walikiwasha kwelikweli na kujibebea ujiko duniani ambapo pia walivaa vitambaa vya unahodha kwa nchi zao hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: