Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida FG: Tupo tayari kuwakilisha Tanzania

Singida Fountain Gate Tizi Singida FG: Tupo tayari kuwakilisha Tanzania

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Singida Fountain Gate FC umeweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Future kutoka Misri.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 17 ikiwa ni hatua ya pili ya awali ya mashindano hayo.

Ofisa Habari wa Singida, Hussein Masanza alisema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo wa kimataifa na maandalizi yapo vizuri.

“Tupo tayari kwa ajili ya mechi yetu ya kimataifa ambayo tutaanza hapa Azam Complex benchi la ufundi linafanya kazi kubwa kufanya maandalizi mazuri ambayo yataleta matokeo mazuri.

“Tunatambua ushindani ni mkubwa nasi tupo tayari kupata matokeo mazuri, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi ili tufanye vizuri kimataifa,” alisema Masanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: