Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yatinga Fainali Kombe la Mapinduzi, Ally Salim aibuka Shujaa

IMG 6474.jpeg Ally Salim, Golikipa wa Simba aliokoa Penati tatu

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Simba SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada y ushindi wa penalti 3-2 dhidi ya Singida Fountain Gate leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.

Singida Fountain Gate ilitangulia kwa bao la mshambuliaji Mkenya Elvis Rupia dakika ya 11, kabla ya kiungo Mkongo Fabrica Luamba Ngoma kuisawazishia Simba SC dakika ya 90 na ushei.

Na kwenye mikwaju ya penalti kipa wa Simba SC, Ali Salim aliyeokoa penalti za mabeki Gardiel Michael, Hamad Waziri na mshambuliaji Mnyarwanda Meddie Kagere kuipa Simba tiketi ya Fainali Kombe la Mapinduzi.

Waliofunga penalti za Simba ni viungo Luis Jose Miquissone, raia wa Msumbiji, Israel Patrick Mwenda na Moses Phiri, wakati ya Shomari Kapombe iliokolewa na ya Mrundi, Saido Ntibanzokiza ikagonga mwamba wa juu na kwenda nje.

Ni viungo, Mkenya Duke Abuya na mzawa, Deus Kaseke pekee waliofunga upande wa Singida Fountain Gate.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: