Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yathibitisha kuachana na Kramo: "Hayupo kwenye mipango yetu"

Kramo Fiti(2) Aubin Kramo.

Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imesema kuwa nyota wao, Aubin Kramo hayupo kwenye mipango ya Simba kwa msimu wa 2024/25 kwa sababu ya tathimini ya kimatibabu na kiufundi kuona hataweza kuwezana na presha ya mashabiki wa Simba kwa msimu mpya.

Hayo yamebainishwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally wakati akizungumzia mambo mbalimbali kuhusu klabu hiyo hasa wachezaji ambao hawajaripoti kambini nchini Misri mpaka sasa akiwemo nyota huyo raia wa Ivory Coast.

“Kramo ametoka katika majeraha makubwa na kutokana na msimu huu utakuwa wa presha kubwa tumeona bora kumtafutia timu aende kwa mkopo au kuachana naye. Maana hataweza presha za mashabiki wanachokihitaji ni ubingwa tu,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: