Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafunguka kumtambulisha kocha mpya

Ahmed Ally Press Leo.jpeg Simba yafunguka kumtambulisha kocha mpya

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klanbu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa viongozi wa klabu hiyo bado wanaendelea na mchakato kumtafuta kocha mpya atakayerithi mikoba ya Robertinho aliyetimuliwa wiki iliyopita.

Ahmed amesema hayo leo Novemba 16, 2023 wakati akizindua kampenzi ya hamasa kuelekea mchezo wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Novemba 25, katika Dimba la Mkapa.

“Kikosi bado kipo chini ya Selemani Matola na cadena wakati viongozi wa juu wakiwa kwenye mchakato wa kumtafuta kisha kumtangaza kocha mkuu mpya. Malengo yetu ni kufanya haraka iwezekanavyo kumpata kocha mpya.

“Tuna shughuli pevu ya back to back, baada ya ASEC kuja hapa, tukimalaizana nao tutakwenda Botswana, kwa hiyo lazima tumpate mwalimu mapema ili kuja kufanya maandalizi kuelekea mechi hizo. Niwaambie muda si mrefu mchakato utakamilika.

“Tunafanya kazi hii kwa umakini ili kumpata mwalimu mwenye sifa zote za kuja kuifundisha Simba. Nyote mnajua tupo katikati ya mashindano, lazima tupate mwalimu ambaye yuko active sio wa kujitafuta tafuta. Tunataka mwalimu akifika aanze kazi moja kwa moja kwa hiyo muda si mrefu tutampata na kumtangaza kisha kumkabidhi Simba yake.

“Hatuwezi kutaja CV za makocha yatabaki kuwa mambo ya ndani. Huu mkutano ilipaswa tuwe na CEo lakini anaendelea na mchakato wa kuangalia nani tumkabidhi Simba Sc. Tuwape muda viongozi ya kutafuta mwalimu.

“Hata sisi hatupendi kuona hatuna kocha, tunataka kocha aje mapema, tumkabidhi timu mapema na aanze kazi mapema mambo yaende. Hakuna kiongozi wa Simba ambaye anapata usingizi timu ikiwa haina kocha, tunataka mwalimu kweli kweli sio wa kuziba nafasi iliyo wazi,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: