Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba waiwahi Yanga dili la Awesu

Awesu Awesu 200.jpeg Kiungo Awesu Ali Awesu

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SAA chache baada ya kuibuka kwa tetesi kwamba Yanga imeamua kuingilia kati dili la usajili wa kiungo Awesu Awesu aliyetambulishwa na Simba kabla ya kutangazwa kurudishwa klabu ya KMC, taarifa mpya ni kwamba mabosi wa Msimbazi wameamua kumkomalia na muda mchache mambo yatatiki.

Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF, iliyosikiliza shauri la KMC kuilalamikia Simba kumchukua mchezaji huyo kinyemela na kumpeleka kambini Misri, iliweka bayana kwamba kuwa Awesu ni mali hali wa Wana Kino Boys ambao walitoa msimamo wanaomhitaji nyota kiungo huyo milango wazi.

Hatua hiyo inalezwa iliwafanya Yanga kutaka kuitibulia Simba kwa kudaiwa kuweka ofa ya Sh150 milioni kwa KMC na viongozi walikuwa wakiendelea kujadiliana, lakini ghafla upepo umebadilika kwa mmoja wa vigogo wa klabu hiyo ya Kinondoni kusema wapo hatua ya mwisho ya kumalizana na Simba.

Kagera Pict

Inaelezwa Simba imeshtuka na kufanya chapu kurudi KMC ili kumalizana na klabu hiyo, kwani licha ya kutangaza kumrejesha kikosini, lakini Awesu alitia mgomo na inadaiwa alikuwa akiendelea na mazoezi na kikosi hicho kwani moyo wake upo huko kwa sasa.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungula aliliambia Mwanaspoti muda mchache uliopita kwamba walikuwa wamefikia pazuri kumalizana na Simba walioamua kurudi kwao ili kumsajili kwa taratibu zilizopo kiungo huyo wa zamani wa Madini FC, Azam na Kagera Sugar.

"Japo nipo nje ya ofisi, ninachojua Simba imefikia hatua za mwisho kulimaliza dili hilo, kutokana na kukaa pande zote mbili ili kufikia mwafaka wa jambo hilo," amesema Mwakasungla na alipoulizwa juu ya ishu ya Yanga kuingiza mkono kuwatibuliwa watani wao amejibu kuwa, hafahamu kuhusiana na ofa hiyo, isipokuwa kinachoendelea Simba na KMC, ili kumalizana kabla ya saa 6:00 usiku.

"Kuhusu Yanga sijafahamu, taarifa za awali ni za Simba kukaa pamoja na uongozi wa KMC, ili kumalizana na jambo hilo kwa taratibu zinazotakiwa."

Hata hivyo, Mwakasungula hakufunguka dau ambalo Simba, wameliweka mezani ili kumuachia mchezaji huyo, ambaye walikuwa kwenye mvutano naye, baada ya kuonekana awali alisaini Simba kimakosa.

Siyo mara ya kwanza kwa Awesu, kuhusishwa kutakiwa na Yanga, kwani tangu msimu uliopita zilikuwa tetesi hizo na hata kwenye dirisha hilio linalofungwa usiku alitajwa pia kutakiwa na Vijana wa Jangwani kabla ya kuibukia Simba.

Hata hivyo, chanzo cha ndani kutoka KMC kinasema kuwa, Simba ilienda na Sh 100 milioni, badala ya Sh 200 Milioni zilizotangazwa awali na klabu hiyo aliyokuwa akiichezea Awesu na kutakuiwa kuongeza Sh 50 milioni na ndipo mazungumzo yakafanyika kabla ya kuzuka kwa tetesi kwamba Yanga nayo imejitosa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: